Wednesday, 28 January 2015

AINA ZA MADIRA

Kuna aina mbalimbali za madira kuna yanayovaliwa nyumbani,harusinina mazikoni.


ra ya harusini

Maua ya bi harusi

Bi harusi anapokwenda holini huvaa vizuri na hubeba maua kwa kuashiria upendo kwa mumewe.


ua la bi harusi

Saturday, 17 January 2015

ATHARI YA MADAWA YA KULEVYA.

Kenya na Tanzania zapiga marufuku na kuweka sheria mpya ya uvutaji shisha

(GMT+08:00) 2014-07-17 17:32:21
Uvutaji wa kilevi kipya kinachojulikana kama Shisha nchini Kenya na Tanzania unaendelea kukuwa kwa kasi na kuwateka vijana wengi. Kufuatia tabia hiyo uvutaji wa shisha, serikali ya Kenya pamoja na ile ya Tanzania kupitia idara husika zimeamua kuchukua hatua za kupiga marufuku na kuweka sheria mpya. Hatua hii imechukuliwa kutokana na onyo kutoka kwa wataalamu wa afya walioeleza kuwa kilevi hicho kina athari kubwa zaidi ya uvutaji wa sigara. Nchini Kenya, shisha ndio mtindo mpya wa vijana wanaotumia kujiburudisha katika vilabu vya burudani. Wake kwa waume hukusanyika katika vilabu na kuvuta kwa vikundi aina tofauti za shisha bila kujua athari zake kwa afya zao. Kulingana na mwenyekiti John Mututho, Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la kupambana na mihadarati na dawa za kulevya NACADA pamoja na serikali umebaini kuwa baadhi ya aina za shisha zina viwango fulani vya vileo aina ya Heroine na bangi na cocaine. Mkurugenzi wa NACADA Fazul Mohamed, anasema hali hii imepelekea shirika hilo kupiga marufuku uvutaji wa aina 19 za shisha nchini Kenya zinazosemeka kuwa na viungo vya dawa za kulevya. "Shisha imegundulika kuwa na asilimia kubwa sana ya viwango vya dawa zilizopigwa marufuku na serikali ya Kenya kama heroine. Wavutaji wa shisha wanakuwa hawawezi kuikosa kwa sababu ina vileo hivyo hatari." Anafafanua Bw. Fazul Mohamed Shirika hilo pia limetoa onyo kwa yeyote ambaye atapatikana akivuta au kuuza shisha zilizopigwa marufuku atatiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka. "Yeyote atakaepatikana anavuta ama anauza shisha atakabiliwa na mashtaka kisheria." Nchini Tanzania, wizara ya afya imesema Tanzania inatathmini sheria ya sasa kuhusu matumizi ya Shisha ili kufanya mageuzi au kubadili sheria hiyo. Waziri wa Afya, Dk Seif Rashid amesisitiza kuwa serikali haiungi mkono matumizi ya shisha kwani inafahamu kuwa ni kilevi hatari pengine kuliko sigara za kawaida na pombe. Waziri huyo amesema hawawezi kuwakamata watumiaji lakini wanatafuta mbinu ya kudhibiti kilevi hicho. Kama ilivyo Kenya shisha imepata umaarufu mkubwa nchini Tanzania hususan Dar es Salaam. Taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa, mkupuo mmoja wa shisha, una kemikali hai 4,800 na kwamba kemikali hizo husababisha saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa upumuaji. WHO inaeleza kuwa, kiasi cha uvutaji wa shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara 100 au 200. Wataalamu wa afya wameonya kwamba ulevi huo ambao kwa sasa umeshika kasi na kuteka watu wengi hasa vijana, una hatari kubwa kuliko uvutaji wa sigara Daktari wa masuala ya afya nchini Tanzania Meshack Shimwela anasema ni vizuri watumiaji wakajua madhara ya shisha, badala ya kuchukulia kuwa ni mtindo wa maisha tu au starehe isiyo na madhara. Kwa upande wake Profesa Twalib Ngoma, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Tanzania, anaonya kuwa asilimia 40 ya saratani zote nchini Tanzania zinasababishwa na matumizi ya tumbaku na shisha ina tumbaku. "Shisha imeanza kuwa mtindo mpya kwa vijana, utafiti kuhusu athari zake ulifanywa hivi majuzi na kugundulika kuwa na madhara makubwa. Vijana wengi wanashindwa kuamini athaari zake. Kwa hivyo kwanza lazima jamii ielimishwe kuhusiana na uvutaji wake." Anasema profesa Twalib Ngoma Hata hivyo kwa vijana wengi wanaotumia shisha nchini Kenya na Tanzania wana mtazamo tofauti. Wengi wao wanaimani kuwa kiingiacho mjini sio haramu. John Ndigile anaeleza kwamba yeye na wenzake wanaamini shisha haina madhara kwao, wanaiona kuwa ni kiburudisho kinachowapa faraja kama wavutaji wa sigara na kwamba hamu ya kuvuta kila mara imewaingia. "Shisha ni kama njia moja ya kujipumbaza. Ina ladha tofauti.Wakati tunatumia tunawekewa katika chombo.Tunavuta moshi wake." "Mara ya kwanza nilivuta Shisha eneo la buruburu na nikaona ni nzuri." "Kama nataka kuchangamka huwa navuta Shisha na nikivuta akili yangu huwa inafunguka na Napata uchangamfu. Uvutaji wa shisha una gharama kubwa sana ya kifedha katika sehemu mbalimbali jijini Nairobi. Shisha huuzwa kati ya shiingi elfu 1 hadi elfu 6 kulingana na klabu au sehemu inapouzwa kwa matumizi ya saa moja. Shisha huwekwa ladha kadhaa kama vile vanila, strawberry, mint, chocolate au kahawa ili kuwavutia wavutaji. Kadhalika wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu, kwa makundi hujikusanya na kuchanga fedha kwa ajili ya kuvuta shisha haswa wakati wanapofunga shule. Wateja wakuu ni vijana kati ya umri wa miaka 14 na 45. Shisha ni jina lenye asili ya Misri (sheesha) lenye maana ya bomba la maji lililounganishwa kwenye chombo. Ina hewa ya carbon monoxide ambayo huingia kwenye mapafu na kuchukua nafasi ya hewa safi ya oxygen, hivyo ogani muhimu kuharibika. Shisha ina wingi wa nicotine, kiwango cha kemikali kinachosababisha mishipa katika ubongo kuhisi kupata faraja na raha ya kipekee Hutumiwa sana katika nchi za Misri India na Uturuki.





 
MUATHIRIKA WA MADAWA YA KULEVYA.

Wednesday, 14 January 2015

PIKO

UCHORAJI WA MAUWA YA PIKO.

mauwa ya hina

harusi

PICHA YA SHEREHE
harusi za \anzibar.
picha za asili za mavazi ya biharusi


Harusi  Zanzibar
 

ngoma zetu

ngoma zetu za asili  Zanzibar.





 

Ngoma zetu

wazanzibari tunaringia utamaduni wa ngoma za asili ambazo hadi leo kuna vijiji wanaendeleza ngoma hizo.kwa mfano:mkurungu,boso,mkugo,mwanandege n.k.

mfano wa picha za ngoma hizo ni:


ngoma zetu za asili

kuna ngoma mbalimbali ambazo ni za asili hapa kwetu Zanzibar.kama vile mkurunga,boso,msewe n.k.
picha zinazoonesha wacheza ngoma mbalimbali.

Tuesday, 13 January 2015

mapishi

mapishi ya kizanzibari

udhalilishaji wa wanawake

udhalilishaji wanawake sasa basi kwani tuna haki zetu .MH.doc Ali Mohd Shein anasisitiza kupitia vyombo vya habari .kwa hiyo kama wapo wanaume ambao bado wanadhalilisha wake zao waripotiwe tusiwaonee muhali pindipo utamuona jirani yako anamdhalilisha mkewe na wewe ukakaa kimya utakua umechangia kwa namna moja au nyengine udhalilishaji huo.jamani sote tuungane kukomesha udhalilishaji wa wanawake nchini Tanzania.